FILM TRAILER CLOUDS 112 (DR MAX)

NEW VIDEO FREDRIGO - NAJIULIZA

Showing posts with label BONGO NEWS. Show all posts
Showing posts with label BONGO NEWS. Show all posts

Thursday, November 21, 2013

HUYU NDIE MSANII WA KIKE ALIYE TANGAZA KUUZA NGUO ZAKE;

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
6:07 AM

Msanii wa kike nguli kutokea visiwani zanzibar anefanya music miondoko ya Bongofleva Jamila Abdallah AKA Baby j, ametangaza kuanza kuuza nguo zake mwenyewe, kupitia ukurasa wa page yake ya Facebook Msanii huyo aliandika kuhusiana na kuanza biashara ya kuuza nguo ambazo zitakua zikitoka hapa nchini na nchi za nje,msanii huyo anaemiliki blog yake mwenye yenye shehena ya nyimbo zake Iambabyjay.blogspot.com ,
Baby j amesema music ni pati ya maisha yake lkn pia pia Biashara ni kitu ambacho kipo kwenye damu yake pia, so ameamua kufanya Biashara ya nguo Kupitia Babyj's Clothe Line:
Alipo ulizwa na mwandishi wetu kwa njia ya simu baby j alisema, kwa sasa ameanza na T-shirt ambazo soon zitadondoka mtaani ''kati ya wiki hii ama ifuatayo nita introduce Flana maalum kwa ajili ya kuuza, so watu wasubirie naamini zitakua za kipekee coz timu yangu inajituma kuhakikisha vitu vizur vinapatikana, ni T-shirt ambazo zitanitambulisha kwenye Biashara ya Nguo''  na pia kuna vitu kibao ambavyo vyengine ni kutoka nje ya nchi, so inabidi kuvisubir kwa muda kidogo lkn vikifika atavitangazia kwani anaamini kua Licha ya music kuna maisha pia hivyo bac ni muziki na maisha: alimalizia Baby j:

Kila la Kheri Baby j tunazisubir kwenye Biashara hiyo ya Pamba kwa hamu izo pamba tutinge mitaani:
TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

WOLPER AWAJIBU WANAOMSEMA ANAJIONESHA KI FEDHA:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
12:51 AM

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa Filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amesema kuwa ni mtu mwenye mapenzi kwa wengine wanaokumbwa na matatizo katika jamii mara nyingi amekuwa akisaidia watu kwa kutoa michango kwa wale walio na matatizo na wanahitaji msaada basi yeye uguswa na kuwasaidia.
Wolper amekuwa mstari wa mbele katika harambe mbalimbali hasa pale anapooalikwa na kudhuria katima matamasha yanayohusu wasanii na hata wale ambao si wasanii katika shughuli zao na kutoa michango ambayo yeye anasema ujisikia kutoa japo kuna watu wanaweza kuwa na fedha zaidi yake.
“Suala la kutoa kama tunavyoambia hata katika vitabu vya dini ni moyo wa utoaji kuna watu ambao wana fedha kuliko hata mimi lakini wanaweza kuwa wazito katika utoaji kwa ajili ya kuwasaidia wengine, lakini kwangu nikitoa najisikia amani katika moyo wangu,”anasema Wolper Gambe.
Msanii huyo nyota katika tasnia ya filamu Bongo hivi karibuni alitoa ahadi ya milioni 2 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule ya watoto katika kanisa la KKKT- Kijitonyama, Wolper ndio alikuwa msanii pekee alimchangia mwigizaji mwenzake marehemu Sajuki milioni 16 ili akatibuwe nchini India.


TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

EXCLUSIVE KUHUSU MINI ZIFF 2013 NA FILAMU ZA BONGO:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
12:43 AM

MINI ZIFF 2013 inafanyika sambamba na Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tamasha hili dogo litafanyika tarehe 10 -12 Jan, 2014 na kama kawaida ZIFF itatoa tuzo 10 za Filamu kwa waliofanya vizuri kwa mwaka 2013 katika filamu za Kiswahili (Bongo Movie). Tuzo zitakazotolewa ni Muigizaji Bora wa Kiume na Kike, Muongozaji Bora, Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji anayechipukia, Filamu bora katika Sauti, Filamu bora katika Hadithi, Balozi bora wa Filamu za kitanzania, Kampuni au mtu aliyetoa mchango mkubwa katika Tasnia hii kwa mwaka huu na Tuzo ya Heshima. Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania peke yake (Bongo movies) ilikuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili ni utangulizi wa tamasha kubwa la ZIFF litakalofanyika 14 – 22 Juni, 2014.

Tuzo zitatolewa baada ya jopo la majaji kupitia kazi zilizoletwa kwaajili ya Mini ZIFF na pia Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume na Kike zitapata kupigiwa kura na wananchi kupitia namba maalum itakayotolewa hapo baadae kupitia Puch Mobile na hivyo kufanya watu wote Tanzania nzima kupiga kura.
Mini ZIFF itaonesha filamu kwa siku mbili na siku ya mwisho Tuzo zitatolewa kwa walioshinda, pia tunategemea kuwaalika wasanii mbalimbali maarufu kutoka hapa Tanzania kama JB, Cloud, Steve Nyerere, Ray, Makombora, Simon Mwakifamba, Monalisa, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Lulu na wengine wengi.
Pia tunategemea kufanya show kabambe ya muziki baada ya kutolewa kwa tuzo, wasanii watakaopanda jukwaani watatangazwa hapo baadae. Kwa wale wote wanaotaka kuleta kazi zao basi walete sasa ila ziwe ambazo zimetoka mwaka 2013 tu. Wasiliana na Ibra 0713300997(DAR) au Mohd 0778685676 (ZNZ).
MINI ZIFF 2013 inaletwa kwa udhamini mkubwa wa ZUKU, Push Mobile, Azam Marine, Filamu Central Clouds TV kupitia kipindi cha Take One na Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena.

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Saturday, November 9, 2013

HIZI NDIO SIMU MPYA ZA iPHONE ZINAZOWEZA KUPIMA JOTO RIDI

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
2:58 AM

posted by TimeFm
Inder Singh ameutumia ugonjwa wake wa ini kama fursa ya kugundua kitu kipya na kikubwa katika dunia hii, ambapo sasa toleo jipya la simu aina ya iPhone halitatumika tu kutoa taarifa za kibenk, kutuma na kupokea pesa ama kuperuzi mitandao.
Ugunduzi wa Inder Singh unaiwezesha simu aina ya iPhone (toleo jipya) kuweza kutumika kupima jotoridi la mwili kama kipimajoto cha hospitali (thermometer) na hivyo kuwawezesha wazazi kujua afya za watoto wao mapema wakiwa nyumbani kwa kutumia simu.
Kipima joto maalum kitapachikwa kwenye iPhone hivyo kuiwezesha simu hiyo kupima jotoridi na kuonesha matokeo kwenye screen, ikiwa ni  pamoja na dalili za ugonjwa kwa mtumiaji.
Kwa hali hiyo inawezesha sio tu kuangalia afya wakati unapima, lakini pia kutunza record ya afya na inaweza kueleza kama unaweza kuwa na homa katika kipindi kifupi kijacho.
Inder Singh ambae aligundua kipima joto hicho maalum wakati akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa ini hivyo kutaka kufahamu afya yake kwa urahisi zaidi, amesema homa ni dalili ya magonjwa mengi hivyo kufahamu jotoridi la mwili kutasaidi watumiaji kufahamu afya zao kabla hawajashambuliwa zaidi na magonjwa.
“Fever is an early sign of illness and I wanted to revolutionise the world's most common medical device.”


TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Thursday, November 7, 2013

BEBE COOL,BOBY WINE WARUDISHA FADHILA KWA JAMII

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
2:04 AM

 Picha/habari  EATV
Wasanii wakali kabisa wa Uganda, Bebe Cool pamoja na Bobi Wine kwa nyakati tofauti wameendelea kuonyesha mioyo yao mikunjufu kwa kurudisha fadhila kwa jamii kwa njia za misaada mbali mbali ambayo wameendelea kuitoa kwa wananchi wa Uganda waliopo katika mazingira magumu.

Bebe Cool ameonekana hivi karibuni akiwa katika shughuli nzito ya kupakia mzigo wa simenti pamoja na maji safi ya kunywa kwa ajili ya msaada kwa wananchi huko Ntinda, wakati kwa upande wa pili Bobi Wine yeye amekuwa akikusanya misaada mbalimbali kutoka kwa makampuni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa huko Kasese na Bududa.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo, moyo huu ambao wasanii hawa wameonyesha umekuwa ni wa kipekee na mfano mzuri wa kuigwa na watu wenye nafasi zao katika jamii, na si wasanii wa muziki tu.

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

SARAHA AWAOMBA KURA WATANZANIA KWENYE AWARDS:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
1:57 AM

Msanii wa muziki wa Bongoflava ambaye anaiwakilisha vizuri Tanzania nje ya mipaka ya nchi, Sa Raha amepata shavu la kuingia katika mashindano ya muziki ya kimataifa yanayofahamika kama Global Rockstar - Music Contest 2013, ambayo yanapambanisha zaidi ya wasanii 73 kutoka nchi 73 tofauti duniani.

Saraha ameingia katika shindano hili kupitia wimbo wake wa Jambazi, na mpaka sasa amefanikiwa kufikia hatua ya 16 bora, ambapo Novemba 16  kutafanyika onyesho kubwa kabisa la kazi za washiriki huko Vienna na mwisho wa siku mshindi wa shindano hili atajipatia zawadi ya dola 10,000 za Marekani.

Kupitia mahojiano yake na eNewz, Saraha amewaomba watanzania kumpigia kura na kumwezesha kushinda mashindano haya kupitia mtandao wa www.global-rockstar.com, ambapo pia itakuwa ni nafasi ya kipekee ya kutangaza zaidi muziki wa Bongoflava duniani.
Source EATV

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Joh Makini: ASEMA TATIZO BONGO FLEVA IMEKUA KAMA BUS:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
1:43 AM

Source Times Fm

Kama unakumbuka kuna wakati wasanii wengi wanaofanya hip hop Tanzania walikataa kujumuishwa kwenye kundi la Bongo Fleva ambalo kwa kawaida lilichukuliwa kama jina lililowakilisha nyimbo za kizazi kipya za hapa bongo zilizoanza kusikika miaka ya 90, na hadi leo kuna wana hip hop ambao hawakubali kabisa kuhusishwa na jina hili ‘Bongo Fleva’. Mweusi Joh Makini yeye hana tatizo kabisa na jina hilo na anaamini linaweza kutumika vizuri kuwakilisha muziki mzuri wa kizazi kipya wa Tanzania, lakini anachoona hakiendi sawa ni pale ambapo kila anaejaribu kuimba anaingia kwenye hili bus la Bongo Fleva.
Joh Makini alifunguka akiwa ndani ya ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times fm, walipoweka mjadala huu mezani akiwa na Saleh Jabir aka Kuvichaka, Dj Ommy na mkali wa RnB Damian Soul.
“Sina tatizo kabisa na hili jina ‘Bongo Fleva’, ni kitu kizuri kwa sababu kama kikisimamiwa kinaweza kuwa ni identity ya muziki ambao unatoka Tanzania.
“Tatizo ni kwamba limekuwa kama treni au basi ambalo kila mtu anaweza kudandia, awe na talent asiwe na talent.” Amesema Mwamba wa Kaskazini.
Amesema kwa hali hii wana hip hop wanaona kama ni shida kukaa kwenye bus moja na watu ambao hawana vipaji.
“Mtu unaona, aaagh..I’m in the same bus with someone...huyu ambae anaibia tu, unaona bora niachie, but Bongo Fleva is a good thing.” That’s Joh Makini.
Joh Makini ameshirikishwa na Damian Soul kwenye ngoma yake mpya ‘Ni Mapenzi’ iliyotambulishwa Jumanne (November 5) kwenye The Jump Off.

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Tuesday, November 5, 2013

SMILE AWAFUNGUKIA WALIOVUJISHA NGOMA YAKE YA ''I MISS YOU''

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
2:07 AM

Mchezo wa kutoka kwa nyimbo za wasanii pasipo na ruhusa za wenyewe, umekua ukishamir sana katika industry ya Music Hapa Tanzania, ni tofauti sana na wenzetu kwa muda mchache tuu wa siku kadhaa wameshalalamika wasanii wengi juu ya suala hili,:
Hii nyengine msanii Smile wa Kichefu Kichefu amelalamika pia hivi jana kupitia acount zake tofouti za mitandao ya kijamii kuhusu kuvujishwa kwa nyimbo yake mpya inayoitwa ''i MISS yu'' Kwa mujibu wa Smile amesema Ngoma hiyo huwenda imetolewa na Uwongozi wa Studio Aliyorecordia  (ZENJI REC),  kwa sababu yeye mwenyewe alikua bado anawasikilizisha Wadau wakubwa wa Music ili watoe comment zao kama itoke ama laa,
Lkn amesema pia kitendo hicho hakitomshusha bali kitazidi kumpandisha juu zaidi:
cheki hapa chini alichoandika kutoka kwenye moja ya Account zake:

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Sunday, November 3, 2013

WADAU WAPENDEKEZA KUWEPO NA DIAMOND PLATNUMZ DAY:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
1:52 AM

Kuna uwezekano mkubwa kwamba Diamond Platnumz ni mmoja kati ya Watu waliyo washtua Vijana wengi kwenye maswala ya Mapenzi Kwa wazazi wao hasa mama,  jinsi ya kutokata tamaa kutokana na maisha magumu, na mengine hii yote imetokana kwa uwazi wa maisha ya Diamond Platnumz, Ambao kila mmoja anauelewa tangaua alivyoanza na mpaka sasa alipofikia,
Mmoja kati ya wajasiriamali wa Tanzania anaeishi U.S.A kwa sasa Mohammed Don a,k,a Shangrellah1988 kupitia account yake ya Instagram aliandika kwa kuweka suggetion hilo la hoja ya kuwekwa DIAMOND PALATNUMZ DAY, ya kila mwaka aliandika hivyo.wakati akisifia Juhudi za Kijana Diamond:
Bila ya hiyana kwa kukubali love kutoka kwa Jamaa huyo alijibu Kupitia hapo hapo kwa kuandika:
Swali ni je Unafkir Diamond amewakomboa Vijana wengi Kimawazo Pamoja na kujitambua na je upo umuhimu wa kuwepo kwa DIAMOND PLATNUMZ DAY kila mwaka?????? Mawazo yako Please weka hapo chini-:
TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Saturday, November 2, 2013

(PICHA) HII KALI MAITI WAFUFULIWA KUBADILISHWA NGUO:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
1:35 AM

Nchini indonesia katika kijiji cha Tana Toraja, maiti huwa zinafufuliwa na Kubadilishwa nguo, zoezi hili hufanyika kila mwaka baada ya maiti kuzikwa, na wanafamilia ndio huifanya kai iyo;
Mara nyingi mtu anapo kufa huwa wanamzika katika sehemu aliyo zaliwa na sio aliyokufia so kila baada ya mwaka humfukua na kumbadilisha mavazi, hii ni moja kati ya mila zao wenyewe:
Duuh hii nouma sana mimi kwa hapo neno sina khaa!!!
TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Tuesday, October 29, 2013

RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU MZEE SEPETU:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
2:28 AM

 (Habari imetoka Cloud112.blog)
''Habari zenu ndugu zangu, i hope mmeamka salaama salamin, kwa wale wagongwa allah atawaafu inshaallah:
Tangu juzi nimekua nikishare na nyinyi taarifa za Msiba wa Baba Mzazi wa Mwanafilamu mwenzangu WEMA SEPETU mzee ABRAHAM SEPETU:
Taarifa hizi nazipata kutoka kwa Ndugi wa Karibu wa Wema Sepetu ambae ni Binamu yake anaeitwa RAY ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya Cococnut Zanzibar;
Ratiba YA Mazishi yatakavyo kua Kisiwan Zanzibar:
''Maiti itaondoka na Boti ya Kesho Asubuhi kuelekea Zanzibar na Kufikishwa Moja kwa moja kanisani kwa misa fupi kisha baraza la wawakilishi la Zamani, kwa waheshimiwa kutoa heshima zao za mwisho.Baada ya hapo msafara utaelekea nyumbani kwake Mbuzini kwa ajili ya Mazishi:''
kama kuna chcochote kitakacho badilika tutajulishana hapa hapa:
Ahsanteni Endelea kutembelea blog hii na Uwaambie wengine pia: ''
R.I.P Mzee Abraham Sepetu
TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Sunday, October 27, 2013

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU MZEE ISSAC SEPETU:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
3:19 AM

Hii ni historia fupi na nyazifa alizowahi kushika Baba wa Msanii Maarufu wa Filamu Wema Sepetu Marehemu Mzee ISSAC SEPETU,(pichani)
Jina kamili ISSAC ABRAHAM SEPETU aliwah kusika nafasi ya Ubalozi na ndio maana ni maarufu ka aBalozi Sepetu:
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarag Nyerere.  Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere.
Pia, Machi 27, mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dr Mohammed Shein,  kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitegauchumi ya Zanzibar (ZIPA).
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.

R.I.P ''ISSAC ABRAHAM SEPETU''

TOA POLE ZAKO HAPA KWA FAMILIA MZEE SEPETU:


Bofya like hapa show love:

TAARIFA JUU YA KIFO NA MAZIKO YA BABA WA WEMA SEPETU (MZEE ISSAC SEPETU)

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
2:11 AM


Leo mapema tumepokea taarifa za kifo cha Baba mzazi wa Msanii nguli wa Filam nchini Tanzania Wema Sepetu Mzee Issac Sepetu (pichani), Ambae alikua anaumwa na amelazwa katika hospitali ya TMJ jiji Dar,Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Band Ya #COCONUT BAND ya Zanzibar Bwana RAY ambae ni  ndugu na wema sepetu ba mkubwa kwa ba mdogo, alisema mwili wa mzee sepetu kwa sasa umeshapelekwa katika Monchwari ya hospital Kuu ya Muhimbili:
Alipotakiwa kusema kuhusu wapi na nilini atazikwa mzee huyo: Bw; Ray alisema
Ray Mkurugenzi wa Coconut Band Zanzibar:
''kwa sasa tunawasubiri baadhi ya watoto wake waliyokuwepo marekani wafike, na wengine waliyokuwepo ujerumani na tunatarajia watafika kwenye jumanne, sasa wakifika tutazika kati ya juma nne au juma tano, na mzee tunatarajia atazikwa kwenye shamba yake Visiwani Zanzibar iliyoko shamba Mbuzini''

R.I.P MZEE SEPETU:
TOA ''R.I.P'' ZAKO HAPA KWA MZEE SEPETU


Bofya like hapa show love:

(PICHA)CHECK ALIVYO VAA DIAMOND KWELI SHOW ALIIPANIA:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
12:30 AM

Jana ilikua ni Funga mwaka na Serengeti Fiesta Dar kwenye viwanja vya Leaders club, ambapo zaid ya wasanii 40 walikuepo kuperform siku ya jana, lakini kutokana na hit lafu za Umeme zilizotokea maeneo hayo zilisababisha show kuisha kabla ya  baadhi ya wasanii kama Davido,Mahombi, Daimond na wengne kuwa bado hawaja fanya Vitu vyao stajini,
Kwa Mujibu wa Baadhi ya Mashabiki wa msanii nguli T.z Diamond Platnumz wamesema inawezekana haikufaniakiwa kwa sababu mkamia maji hayanywi:
''aah Diamond aliipania hii show maana si mchezo hayo mavazi aliyotupia ni balaa, pengine alikamia maji ndo maana'' alisema msanii mmoja aliyekuwepo Backstage

Hata ivyo kwa taarifa ni kwamba show iyo inarejewa lewa kwa BURE kabisa katika Viwanja vile vile na Staji lile lile na wasanii wataka panda ni wale waliyokosa kupanda jana, akiwemo  Diamond Platnumz:
SWALI la wengi ni je DIAMOND ataibuka na Mavazi Mapya au Yale yale ya Jana:???
MAONI yako HAPO CHINI

KWA MTAZAMO WAKO WEWE UNASEMAJE KUHUSU HICHO KIKOSI;

Bofya like hapa show love:

Saturday, October 26, 2013

HAWA NDIO WASANII WATAKAO FANYA SHOW BURE LEADERS LEO:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
11:42 PM

(Picha Story na Bongo5)
Kutokana na kutokea hitilafu ya umeme Alfajiri ya leo kwenye show ya Serengeti Fiesta Dar, iliyopelekea baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajia kupanda jukwaani kutumbuiza akiwemo Davido, Mohombi, Diamond, Nay wa Mitego na wengine kushindwa kupanda, leo kuanzia saa tisa, wasanii hao watapanda tena jukwaani kuzikonga nyoyo za mashabiki wao bila kiingilio chochote.

Ni katika uwanja ule ule, jukwaa lile lile la Serengeti Fiesta Dar es Salaam ambapo Diamond,Davido,Mohombi pamoja na Nay wa Mitego watapanda kuanzia saa 9 jioni mpaka saa 12.

Show hiyo ya bure itapambwa pia na bendi ya Twanga Pepeta.
TOA MAONI YAKO HAPA:
KWA MTAZAMO WAKO WEWE UNASEMAJE KUHUSU HICHO KIKOSI;

Bofya like hapa show love:

SABABU ZA DOGO JANJA KUTIMULIWA NA OSTAZ JUMA:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
3:03 AM

'''Baada ya siku ya jana kupatikana kwa habari za Dogo Janja kutimuliwa kundi la Watanashati Entertinment lililo chini ya uongozi wa kwa utovu wa nidhamu na tabia mbaya ambayo dogo Janja alikuwa ameianzisha. Tofauti na wengi walivyodhani kuwa Dogo Janja atarudi kwa Arusha na maisha yatasonga lakini imekuwa sivyo, Dogo janja alielwa kosa lake na kuamua kuomba msamaha katika Uongozi wa Watanashati na kukubaliwa na kurudi kundini kama zamani, Mtoto akinyea mkono huwezi kuukata ila utaosha na maisha yataendelea kama kawaida, hii ndiyo falsafa aliyoitumia Ostaz Juma Namusoma kwani anamchukulia Dogo Janja kama mwanae au mtu wake wa karibu;''
(imeandikwa na teamsolothang blog) TOA MAONI YAKO HAPA:
KWA MTAZAMO WAKO WEWE UNASEMAJE KUHUSU HICHO KIKOSI;

Bofya like hapa show love:

DUUUH HUU NDIO MSHAHARA WA MZEE MAJUTO KWENYE FILAMU:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
12:06 AM

 (imetoka BONGOMOVIES)
Umeshawahi kujiuliza Mzee Majuto anaweza kuwa anaingiza shilingi ngapi kwa kuigiza kwenye movie zake za vichekesho ambazo mpaka sasa ndio zinashika namba 1 kwa mauzo Tanzania?
Akizungumza na mtandao wa millardayo Mzee majuto amesema ‘kwenye movie za kuigiza sasa hivi kama mtu akitaka kunishirikisha ni lazima unilipe milioni nane kutoka milioni 2 au tatu nilizokua nazikusanya mwanzoni, hii bei nimeibadili kuanzia mwezi September 2013, mimi kadri ninavyocheza movie nyingie za kushirikishwa ndio nazidi kujipunguzia kipato changu kwa mwezi kutoka kampuni ya STEPS iliyoniajiri’
‘Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 toka nimeanza kuigiza za kushirikishwa na zangu mwenyewe, nilianza kulipwa zaidi ya milioni moja kwenye movie toka mwaka 2007/2008 baada ya kuwa na kampuni ya Ally Riyami ambae alikua ananilipa shilingi laki sita kwa kila movie ya Comedy kwa hiyo kwa mwezi napata mpaka kwenye milioni 6 au saba kutokana na idadi ya movie nitakazoigiza’ – Mzee Majuto
‘kwa sasa hapa Steps nalipwa kuanzia milioni 17 mpaka 20 kwa mwezi, ni malipo mazuri sana ambayo napata kila mwezi na nimepangiwa kucheza movie 9 kwa mwaka lakini kule Ally Riyami kwa mwezi ndio nilikua nacheza hizo movie 10, yani unacheza movie nyingi mpaka unasikia kizunguzungu…. kwa sababu nilitakiwa kucheza movie 1 kila baada ya siku tatu ila kwa sasa kwenye mkataba wa Steps nacheza movie moja ya kampuni na moja ya nje ya kampuni, maisha mazuri’ – Mzee Majuto
HIVI UNAFIKIRI MZEE MAJUTO ANASTAHILI KULIPWA HELA IYO KWA SASA AMA HASTAHILI???? TOA MAONI YAKO HAPA:
KWA MTAZAMO WAKO WEWE UNASEMAJE KUHUSU HICHO KIKOSI;

Bofya like hapa show love:

Wednesday, October 23, 2013

SEHEMU YA KWANZA YA KIPINDI CHA WEMA SEPETU:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
3:26 AM

Kile kipindi kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa filamu nchini , “Wema Sepetu Reality show” kwa mara ya kwanza kimeruka hewani kupitia kituo cha TV cha EATV  hapo jana.
Katika episode hii ya kwanza, Wema amejitambulisha nan  kuelezea historia yake kwa ufupi kukusu yeye.
Lakini pia Wema ameongea mengi sema uvutaji wa sigara, kurogwa ugomvi na dada ake, kuhusu boi wake wa kwanza, amekaa na boi wangapi mpaka sasa, Jinsi walivyoanza na Diamond,kuhusu Kajala, kama hukupata kuicheki iangalie hapa kwa mara ya kwanza:


TOA MAONI YAKO HAPA:
KWA MTAZAMO WAKO WEWE UNASEMAJE KUHUSU HICHO KIKOSI;

Bofya like hapa show love:

Sunday, October 20, 2013

KIANGALIE KIKOSI CHA YANGA KITAKACHO IVAA SIMBA LEO:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
5:29 AM

Kama tujuavyo leo kuna mechi kali sana kati ya wapinzani wa jadi, SIMBA na YANGA, ahadi kede kede zimewekwa na wachezaji pamoja ana mashabiki wa timu hizo mbili, majigambo pia tumeyasikia kutoka kwa wachezaji pamoja ana mashabiki wa timu zote mbili, lakini tunavyoamini sisi ni kwamba mpira Dakika tisini,Kabla hujafika hebu chukua time kuangalia list ya YANGA, itakayoingia uwanjani pamoja na Reserve wake hapa:
 Heres Young Africans line-up to face Simba SC today:
1.Ally Mustapha 'Barthez' - 1
2.Mbuyu Twite - 6
3.David Luhende - 3
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' - 23
5.Kelvin Yondani 'Cotton' - 5
6.Athuman Idd 'Chuji' - 24
7.Haruna Niyonzima - 8
8.Frank Domayo 'Chumvi' - 18
9.Didier Kavumbagu - 7
10.Mrisho Ngassa - 17
11.Hamis Kiiza - 20

Subs:
1.Deogratius Munishi 'Dida' - 30
2.Juma Abdul - 12
3.Oscar Joshua - 4
4.Rajab Zahir - 14
5.Saimon Msuva - 27
6.Nizar Khalfani - 16
7.Jerson Tegete - 10

TOA MAONI YAKO HAPA:
KWA MTAZAMO WAKO WEWE UNASEMAJE KUHUSU HICHO KIKOSI;

Bofya like hapa show love:

Saturday, October 19, 2013

MASHAIRI YA NGOMA MPYA YA SOLO THANG ''MDUDU'';

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
8:01 AM

Baada ya kuamua kustopisha kuachia ngoma yake ya Mdudu,Kwa heshima ya HIP HOP na uzito wa ngoma ya Fareed Kubanda  #SiriYaMchezo, Sasa ameanua aachie Mashairi ya ngoma iyo ambayo Rasmin inatarijiwa Kuachiwa Ijumaa Ijayo Kwa Mujibu wa Solo Thang: Ngoma Ya Mdudu amemshirikisha Mr blue na studio ni CLOUD 9 (BELFAST), DEFATALITY (DSM) Producers SNIPER G GANJI (BEAT),MESSEN (MIXIN & MASTERING)
 Hii hapa Lyrics ya Mdudu: Song utalipata hapa hapa likiachiwa tuuu; tuombe uzima tuu:
usisahau kuweka mstari ulio ukubali kutoka kwenye Lyrics hizi:


iNTro
(DEFA
TALITY MUSIC)
YOU KNOW WHAT TIME IT IS   
ITS YA BOY BACK          (HELLO HELLO HALOOOO)
SOLO THANG                  (ULAMAA)
AAAAAH THIS TIME AROUND
I THINK WE NEED "DUDU KILLER"  (LETS GO NOW)

VERSE 1:
EYO NAKUPA MFANO NJAA ,NA HUYU MDUDU WANAFANANA
SI UNAKULA KILA SIKU ,ILA NJAA INARUDI TENA
MDUDU ANACHEZA NA FEELINGS DAWA KAIIMBA MARVIN GAYE

(SEXUAL HEALING?) , HAUPONI MDUDU YUPO EVERY DAY
SIO KUNGUNI ILA ,NAE ANAPENDA KITANDA
NDIO LOCATION KAMA MOVIE, ACTION- KUNG FU PANDA
YE ANAPENDA NJIA PANDA KAMA UMBO LA MANATI
NDANI YA FIKRA KAKUJAZA KUWA, NISHATI  MIHADHARATI
SIO FUNDI BILA SPANA NA, ANALEGEZA MACHO
HAKITOSHI ULICHONACHO SHARTI UPATE CHA MWENZAKO

YE NDIO CHANZO CHA MAYAI ALIPOMVA KUKU
NDIO KISA JOGOO HUWIKA WEWEEE MAMBO IPO HUKU 
HAICHEKESHI WE UNACHEKA, NDIO UJUE TAYARI
HAKUNYESHI WE UMELOA USIJISHIKE TAFADHALI
NA SIO SHETANI USEME ANAPANDA KWA UBANI 
NA SIO WA KOKWA LA EMBE NAMBIE NI MDUDU GANI??
CHORUS
CHEKI MDUDU ANAVYOWASHAAAAA (washa washa)
ANANIFANYA NINAKUA BWEGE
AKILI ZINAKUA NA MATEGE
ANACHOTAKA NDIO NAFANYA ANACHOTAKA NDIO NAFANYA!!
VERSE 2
SI BORA ANGEKUA PANYA UWEKE SUMU AMA MTEGO
PALE PALE KWENYE SHIMO HAHAAAA NDAGA FIJO
WATU NATEMBEA NA "PUMP" KAMA MAFUNDI BAISKELI
KAZI KUJAZA WATU UPEPO NA "BLADDER' ZINAJAA KWELI

HANA SINDANO SIO DONDORA USEME MPIRA KAUTOBOA
BILA ZANA USICHEZE RAFU, REFA KADI ASIPOTOA?
WE HAMIRA YE NI NGANO LAZIMA MMOJA ANAVIMBA 
OGOPA SANA HUYU MDUDU ANATISHA KAMA SIMBA

KANGA MOJA NDEMBE NDEMBE ETI LAKI SI PESA
NA HAUWEZI KUISHI KAMA BURUDA BROTHER KAKA UTAJITESA
ILA MDUDU AKIKUPA NGOMA NENDA KANUNUE GUITAR
NDIO SAFARI UNAENDA ANZISHA BENDI KAKA FUTI SITA

SIO MBU USEME UTAPATA MALARIA 
YE ANASAMBAZA UGONJWA AMBAO UNAITWA SEX-ERIA
NA SIO SHETANI USEME ANAPANDA KWA UBANI 
NA SIO WA KOKWA LA EMBE NAMBIE NI MDUDU GANI??
CHORUS
CHEKI MDUDU ANAVYOWASHAAAAA (washa washa)
ANANIFANYA NINAKUA BWEGE
AKILI ZINAKUA NA MATEGE
ANACHOTAKA NDIO NAFANYA ANACHOTAKA NDIO NAFANYA!!
VERSE 3
UKIBANWA NA KIKOHOZI, NI LAZIMA UKOHOE
VIPI UKIBANWA NA MDUDU JIBU NENDA KAKOKOTOE
JAMAA KASHIKIWA PANGA AKAAMBIWA LAMBA MCHANGA
AKAGOMA AKATOKA NDUKI BREKI YA KWANZA KWAO UPANGA
JOLY, KAMKUTA DEMU, YULE DEMU AKAONYESHA SHANGA
HADHARA NDIO IKAWA CHUMBA!, MAANA MDUDU KASHAPANDA

SIO KWAMBA ALIKUA NA NJAA, ILA 'SHAWTY" KALA KONI
SI ANA KIU? MPE MAJI SASA BROTHER KULIKONI??
YEAH SIJAPATA KUONA MKATE MGUMU MBELE YA SUPU
VIPI NGOZI ZA UDONGO MZIGANDISHE KAMA SUMAKU?

INGAWA UMBO SIO CHAKULA, WATU UDENDA UNAWATOKA
UTASKIA KASHATAFUNWA, JIULIZE MWILI BANZOKA?
HUU MCHEZO USIO NA DRAW, LAZIMA MTU APIGWE BAO
UCHU KAMA MPENDA NYAMA, HAWA WADUDU NDIO ZAO
NA SIO SHETANI USEME ANAPANDA KWA UBANI 
NA SIO WA KOKWA LA EMBE NAMBIE NI MDUDU GANI?
CHORUS!
CHEKI MDUDU ANAVYOWASHAAAAA (washa washa)
ANANIFANYA NINAKUA BWEGE
AKILI ZINAKUA NA MATEGE
ANACHOTAKA NDIO NAFANYA ANACHOTAKA NDIO NAFANYA!!
 

 
TOA MAONI YAKO HAPA:
KWA MTAZAMO WAKO WEWE UNASEMAJE KUHUSU HILI;

Bofya like hapa show love:

Proudly Powered by Blogger.
back to top