FILM TRAILER CLOUDS 112 (DR MAX)

NEW VIDEO FREDRIGO - NAJIULIZA

Thursday, November 7, 2013

BEBE COOL,BOBY WINE WARUDISHA FADHILA KWA JAMII

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
2:04 AM

 Picha/habari  EATV
Wasanii wakali kabisa wa Uganda, Bebe Cool pamoja na Bobi Wine kwa nyakati tofauti wameendelea kuonyesha mioyo yao mikunjufu kwa kurudisha fadhila kwa jamii kwa njia za misaada mbali mbali ambayo wameendelea kuitoa kwa wananchi wa Uganda waliopo katika mazingira magumu.

Bebe Cool ameonekana hivi karibuni akiwa katika shughuli nzito ya kupakia mzigo wa simenti pamoja na maji safi ya kunywa kwa ajili ya msaada kwa wananchi huko Ntinda, wakati kwa upande wa pili Bobi Wine yeye amekuwa akikusanya misaada mbalimbali kutoka kwa makampuni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa huko Kasese na Bududa.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo, moyo huu ambao wasanii hawa wameonyesha umekuwa ni wa kipekee na mfano mzuri wa kuigwa na watu wenye nafasi zao katika jamii, na si wasanii wa muziki tu.

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

KHAMIS HK (Writer)

My Phone Number :+255718109106,

  • My TWITTER
  • My FACEBOOK

  • 0 comments:

    Proudly Powered by Blogger.
    back to top