FILM TRAILER CLOUDS 112 (DR MAX)

NEW VIDEO FREDRIGO - NAJIULIZA

Thursday, November 21, 2013

HUYU NDIE MSANII WA KIKE ALIYE TANGAZA KUUZA NGUO ZAKE;

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
6:07 AM

Msanii wa kike nguli kutokea visiwani zanzibar anefanya music miondoko ya Bongofleva Jamila Abdallah AKA Baby j, ametangaza kuanza kuuza nguo zake mwenyewe, kupitia ukurasa wa page yake ya Facebook Msanii huyo aliandika kuhusiana na kuanza biashara ya kuuza nguo ambazo zitakua zikitoka hapa nchini na nchi za nje,msanii huyo anaemiliki blog yake mwenye yenye shehena ya nyimbo zake Iambabyjay.blogspot.com ,
Baby j amesema music ni pati ya maisha yake lkn pia pia Biashara ni kitu ambacho kipo kwenye damu yake pia, so ameamua kufanya Biashara ya nguo Kupitia Babyj's Clothe Line:
Alipo ulizwa na mwandishi wetu kwa njia ya simu baby j alisema, kwa sasa ameanza na T-shirt ambazo soon zitadondoka mtaani ''kati ya wiki hii ama ifuatayo nita introduce Flana maalum kwa ajili ya kuuza, so watu wasubirie naamini zitakua za kipekee coz timu yangu inajituma kuhakikisha vitu vizur vinapatikana, ni T-shirt ambazo zitanitambulisha kwenye Biashara ya Nguo''  na pia kuna vitu kibao ambavyo vyengine ni kutoka nje ya nchi, so inabidi kuvisubir kwa muda kidogo lkn vikifika atavitangazia kwani anaamini kua Licha ya music kuna maisha pia hivyo bac ni muziki na maisha: alimalizia Baby j:

Kila la Kheri Baby j tunazisubir kwenye Biashara hiyo ya Pamba kwa hamu izo pamba tutinge mitaani:
TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

WOLPER AWAJIBU WANAOMSEMA ANAJIONESHA KI FEDHA:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
12:51 AM

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa Filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amesema kuwa ni mtu mwenye mapenzi kwa wengine wanaokumbwa na matatizo katika jamii mara nyingi amekuwa akisaidia watu kwa kutoa michango kwa wale walio na matatizo na wanahitaji msaada basi yeye uguswa na kuwasaidia.
Wolper amekuwa mstari wa mbele katika harambe mbalimbali hasa pale anapooalikwa na kudhuria katima matamasha yanayohusu wasanii na hata wale ambao si wasanii katika shughuli zao na kutoa michango ambayo yeye anasema ujisikia kutoa japo kuna watu wanaweza kuwa na fedha zaidi yake.
“Suala la kutoa kama tunavyoambia hata katika vitabu vya dini ni moyo wa utoaji kuna watu ambao wana fedha kuliko hata mimi lakini wanaweza kuwa wazito katika utoaji kwa ajili ya kuwasaidia wengine, lakini kwangu nikitoa najisikia amani katika moyo wangu,”anasema Wolper Gambe.
Msanii huyo nyota katika tasnia ya filamu Bongo hivi karibuni alitoa ahadi ya milioni 2 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule ya watoto katika kanisa la KKKT- Kijitonyama, Wolper ndio alikuwa msanii pekee alimchangia mwigizaji mwenzake marehemu Sajuki milioni 16 ili akatibuwe nchini India.


TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

EXCLUSIVE KUHUSU MINI ZIFF 2013 NA FILAMU ZA BONGO:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
12:43 AM

MINI ZIFF 2013 inafanyika sambamba na Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tamasha hili dogo litafanyika tarehe 10 -12 Jan, 2014 na kama kawaida ZIFF itatoa tuzo 10 za Filamu kwa waliofanya vizuri kwa mwaka 2013 katika filamu za Kiswahili (Bongo Movie). Tuzo zitakazotolewa ni Muigizaji Bora wa Kiume na Kike, Muongozaji Bora, Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji anayechipukia, Filamu bora katika Sauti, Filamu bora katika Hadithi, Balozi bora wa Filamu za kitanzania, Kampuni au mtu aliyetoa mchango mkubwa katika Tasnia hii kwa mwaka huu na Tuzo ya Heshima. Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania peke yake (Bongo movies) ilikuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili ni utangulizi wa tamasha kubwa la ZIFF litakalofanyika 14 – 22 Juni, 2014.

Tuzo zitatolewa baada ya jopo la majaji kupitia kazi zilizoletwa kwaajili ya Mini ZIFF na pia Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume na Kike zitapata kupigiwa kura na wananchi kupitia namba maalum itakayotolewa hapo baadae kupitia Puch Mobile na hivyo kufanya watu wote Tanzania nzima kupiga kura.
Mini ZIFF itaonesha filamu kwa siku mbili na siku ya mwisho Tuzo zitatolewa kwa walioshinda, pia tunategemea kuwaalika wasanii mbalimbali maarufu kutoka hapa Tanzania kama JB, Cloud, Steve Nyerere, Ray, Makombora, Simon Mwakifamba, Monalisa, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Lulu na wengine wengi.
Pia tunategemea kufanya show kabambe ya muziki baada ya kutolewa kwa tuzo, wasanii watakaopanda jukwaani watatangazwa hapo baadae. Kwa wale wote wanaotaka kuleta kazi zao basi walete sasa ila ziwe ambazo zimetoka mwaka 2013 tu. Wasiliana na Ibra 0713300997(DAR) au Mohd 0778685676 (ZNZ).
MINI ZIFF 2013 inaletwa kwa udhamini mkubwa wa ZUKU, Push Mobile, Azam Marine, Filamu Central Clouds TV kupitia kipindi cha Take One na Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena.

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Saturday, November 9, 2013

HIZI NDIO SIMU MPYA ZA iPHONE ZINAZOWEZA KUPIMA JOTO RIDI

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
2:58 AM

posted by TimeFm
Inder Singh ameutumia ugonjwa wake wa ini kama fursa ya kugundua kitu kipya na kikubwa katika dunia hii, ambapo sasa toleo jipya la simu aina ya iPhone halitatumika tu kutoa taarifa za kibenk, kutuma na kupokea pesa ama kuperuzi mitandao.
Ugunduzi wa Inder Singh unaiwezesha simu aina ya iPhone (toleo jipya) kuweza kutumika kupima jotoridi la mwili kama kipimajoto cha hospitali (thermometer) na hivyo kuwawezesha wazazi kujua afya za watoto wao mapema wakiwa nyumbani kwa kutumia simu.
Kipima joto maalum kitapachikwa kwenye iPhone hivyo kuiwezesha simu hiyo kupima jotoridi na kuonesha matokeo kwenye screen, ikiwa ni  pamoja na dalili za ugonjwa kwa mtumiaji.
Kwa hali hiyo inawezesha sio tu kuangalia afya wakati unapima, lakini pia kutunza record ya afya na inaweza kueleza kama unaweza kuwa na homa katika kipindi kifupi kijacho.
Inder Singh ambae aligundua kipima joto hicho maalum wakati akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa ini hivyo kutaka kufahamu afya yake kwa urahisi zaidi, amesema homa ni dalili ya magonjwa mengi hivyo kufahamu jotoridi la mwili kutasaidi watumiaji kufahamu afya zao kabla hawajashambuliwa zaidi na magonjwa.
“Fever is an early sign of illness and I wanted to revolutionise the world's most common medical device.”


TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

HARD MAD AMJIBU JIDE KWENYE YAHAYA ''NAISHI GHETO''

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
12:06 AM

 Msanii Hard mad amewaokoa mAYAHAYA wengi waliyoimbwa na mwanadada Lady Jide, baada ya kuachia hii ngoma ikiwa imejibu maswali yote aliyo uliza Jide kwa Yahaya:

''Jamanii tel jide me no beef no one, naishi ghetto Maskani kweli kinondoni no trouble no one''

Maswali ya Lady jay dee kwenye Yahaya yamemgusa hard mad na kuamua kujivika u- yahaya na kumjibu kupitia ngoma hii yan Naishi Gheto: iskize hapa tumekuekea:
Japo kua mpaka sasa bado haijatambulika kama Lady jay dee alikua na taarifa juu ya ujio huu wa Yahay Rmx kutoka kwa bwana mkubwa Hard mad: Ngoja tuone Jide atasema nini Kuhusiana na hili:

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Thursday, November 7, 2013

BEBE COOL,BOBY WINE WARUDISHA FADHILA KWA JAMII

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
2:04 AM

 Picha/habari  EATV
Wasanii wakali kabisa wa Uganda, Bebe Cool pamoja na Bobi Wine kwa nyakati tofauti wameendelea kuonyesha mioyo yao mikunjufu kwa kurudisha fadhila kwa jamii kwa njia za misaada mbali mbali ambayo wameendelea kuitoa kwa wananchi wa Uganda waliopo katika mazingira magumu.

Bebe Cool ameonekana hivi karibuni akiwa katika shughuli nzito ya kupakia mzigo wa simenti pamoja na maji safi ya kunywa kwa ajili ya msaada kwa wananchi huko Ntinda, wakati kwa upande wa pili Bobi Wine yeye amekuwa akikusanya misaada mbalimbali kutoka kwa makampuni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa huko Kasese na Bududa.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo, moyo huu ambao wasanii hawa wameonyesha umekuwa ni wa kipekee na mfano mzuri wa kuigwa na watu wenye nafasi zao katika jamii, na si wasanii wa muziki tu.

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

SARAHA AWAOMBA KURA WATANZANIA KWENYE AWARDS:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
1:57 AM

Msanii wa muziki wa Bongoflava ambaye anaiwakilisha vizuri Tanzania nje ya mipaka ya nchi, Sa Raha amepata shavu la kuingia katika mashindano ya muziki ya kimataifa yanayofahamika kama Global Rockstar - Music Contest 2013, ambayo yanapambanisha zaidi ya wasanii 73 kutoka nchi 73 tofauti duniani.

Saraha ameingia katika shindano hili kupitia wimbo wake wa Jambazi, na mpaka sasa amefanikiwa kufikia hatua ya 16 bora, ambapo Novemba 16  kutafanyika onyesho kubwa kabisa la kazi za washiriki huko Vienna na mwisho wa siku mshindi wa shindano hili atajipatia zawadi ya dola 10,000 za Marekani.

Kupitia mahojiano yake na eNewz, Saraha amewaomba watanzania kumpigia kura na kumwezesha kushinda mashindano haya kupitia mtandao wa www.global-rockstar.com, ambapo pia itakuwa ni nafasi ya kipekee ya kutangaza zaidi muziki wa Bongoflava duniani.
Source EATV

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Joh Makini: ASEMA TATIZO BONGO FLEVA IMEKUA KAMA BUS:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
1:43 AM

Source Times Fm

Kama unakumbuka kuna wakati wasanii wengi wanaofanya hip hop Tanzania walikataa kujumuishwa kwenye kundi la Bongo Fleva ambalo kwa kawaida lilichukuliwa kama jina lililowakilisha nyimbo za kizazi kipya za hapa bongo zilizoanza kusikika miaka ya 90, na hadi leo kuna wana hip hop ambao hawakubali kabisa kuhusishwa na jina hili ‘Bongo Fleva’. Mweusi Joh Makini yeye hana tatizo kabisa na jina hilo na anaamini linaweza kutumika vizuri kuwakilisha muziki mzuri wa kizazi kipya wa Tanzania, lakini anachoona hakiendi sawa ni pale ambapo kila anaejaribu kuimba anaingia kwenye hili bus la Bongo Fleva.
Joh Makini alifunguka akiwa ndani ya ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times fm, walipoweka mjadala huu mezani akiwa na Saleh Jabir aka Kuvichaka, Dj Ommy na mkali wa RnB Damian Soul.
“Sina tatizo kabisa na hili jina ‘Bongo Fleva’, ni kitu kizuri kwa sababu kama kikisimamiwa kinaweza kuwa ni identity ya muziki ambao unatoka Tanzania.
“Tatizo ni kwamba limekuwa kama treni au basi ambalo kila mtu anaweza kudandia, awe na talent asiwe na talent.” Amesema Mwamba wa Kaskazini.
Amesema kwa hali hii wana hip hop wanaona kama ni shida kukaa kwenye bus moja na watu ambao hawana vipaji.
“Mtu unaona, aaagh..I’m in the same bus with someone...huyu ambae anaibia tu, unaona bora niachie, but Bongo Fleva is a good thing.” That’s Joh Makini.
Joh Makini ameshirikishwa na Damian Soul kwenye ngoma yake mpya ‘Ni Mapenzi’ iliyotambulishwa Jumanne (November 5) kwenye The Jump Off.

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Tuesday, November 5, 2013

SMILE AWAFUNGUKIA WALIOVUJISHA NGOMA YAKE YA ''I MISS YOU''

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
2:07 AM

Mchezo wa kutoka kwa nyimbo za wasanii pasipo na ruhusa za wenyewe, umekua ukishamir sana katika industry ya Music Hapa Tanzania, ni tofauti sana na wenzetu kwa muda mchache tuu wa siku kadhaa wameshalalamika wasanii wengi juu ya suala hili,:
Hii nyengine msanii Smile wa Kichefu Kichefu amelalamika pia hivi jana kupitia acount zake tofouti za mitandao ya kijamii kuhusu kuvujishwa kwa nyimbo yake mpya inayoitwa ''i MISS yu'' Kwa mujibu wa Smile amesema Ngoma hiyo huwenda imetolewa na Uwongozi wa Studio Aliyorecordia  (ZENJI REC),  kwa sababu yeye mwenyewe alikua bado anawasikilizisha Wadau wakubwa wa Music ili watoe comment zao kama itoke ama laa,
Lkn amesema pia kitendo hicho hakitomshusha bali kitazidi kumpandisha juu zaidi:
cheki hapa chini alichoandika kutoka kwenye moja ya Account zake:

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

Proudly Powered by Blogger.
back to top