FILM TRAILER CLOUDS 112 (DR MAX)

NEW VIDEO FREDRIGO - NAJIULIZA

Thursday, November 7, 2013

Joh Makini: ASEMA TATIZO BONGO FLEVA IMEKUA KAMA BUS:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
1:43 AM

Source Times Fm

Kama unakumbuka kuna wakati wasanii wengi wanaofanya hip hop Tanzania walikataa kujumuishwa kwenye kundi la Bongo Fleva ambalo kwa kawaida lilichukuliwa kama jina lililowakilisha nyimbo za kizazi kipya za hapa bongo zilizoanza kusikika miaka ya 90, na hadi leo kuna wana hip hop ambao hawakubali kabisa kuhusishwa na jina hili ‘Bongo Fleva’. Mweusi Joh Makini yeye hana tatizo kabisa na jina hilo na anaamini linaweza kutumika vizuri kuwakilisha muziki mzuri wa kizazi kipya wa Tanzania, lakini anachoona hakiendi sawa ni pale ambapo kila anaejaribu kuimba anaingia kwenye hili bus la Bongo Fleva.
Joh Makini alifunguka akiwa ndani ya ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times fm, walipoweka mjadala huu mezani akiwa na Saleh Jabir aka Kuvichaka, Dj Ommy na mkali wa RnB Damian Soul.
“Sina tatizo kabisa na hili jina ‘Bongo Fleva’, ni kitu kizuri kwa sababu kama kikisimamiwa kinaweza kuwa ni identity ya muziki ambao unatoka Tanzania.
“Tatizo ni kwamba limekuwa kama treni au basi ambalo kila mtu anaweza kudandia, awe na talent asiwe na talent.” Amesema Mwamba wa Kaskazini.
Amesema kwa hali hii wana hip hop wanaona kama ni shida kukaa kwenye bus moja na watu ambao hawana vipaji.
“Mtu unaona, aaagh..I’m in the same bus with someone...huyu ambae anaibia tu, unaona bora niachie, but Bongo Fleva is a good thing.” That’s Joh Makini.
Joh Makini ameshirikishwa na Damian Soul kwenye ngoma yake mpya ‘Ni Mapenzi’ iliyotambulishwa Jumanne (November 5) kwenye The Jump Off.

TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

KHAMIS HK (Writer)

My Phone Number :+255718109106,

  • My TWITTER
  • My FACEBOOK

  • 0 comments:

    Proudly Powered by Blogger.
    back to top