FILM TRAILER CLOUDS 112 (DR MAX)

NEW VIDEO FREDRIGO - NAJIULIZA

Thursday, November 21, 2013

WOLPER AWAJIBU WANAOMSEMA ANAJIONESHA KI FEDHA:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
12:51 AM

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa Filamu Swahiliwood Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amesema kuwa ni mtu mwenye mapenzi kwa wengine wanaokumbwa na matatizo katika jamii mara nyingi amekuwa akisaidia watu kwa kutoa michango kwa wale walio na matatizo na wanahitaji msaada basi yeye uguswa na kuwasaidia.
Wolper amekuwa mstari wa mbele katika harambe mbalimbali hasa pale anapooalikwa na kudhuria katima matamasha yanayohusu wasanii na hata wale ambao si wasanii katika shughuli zao na kutoa michango ambayo yeye anasema ujisikia kutoa japo kuna watu wanaweza kuwa na fedha zaidi yake.
“Suala la kutoa kama tunavyoambia hata katika vitabu vya dini ni moyo wa utoaji kuna watu ambao wana fedha kuliko hata mimi lakini wanaweza kuwa wazito katika utoaji kwa ajili ya kuwasaidia wengine, lakini kwangu nikitoa najisikia amani katika moyo wangu,”anasema Wolper Gambe.
Msanii huyo nyota katika tasnia ya filamu Bongo hivi karibuni alitoa ahadi ya milioni 2 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule ya watoto katika kanisa la KKKT- Kijitonyama, Wolper ndio alikuwa msanii pekee alimchangia mwigizaji mwenzake marehemu Sajuki milioni 16 ili akatibuwe nchini India.


TUMIA FACEBOOK KUTOA COMMENT HAPA:


Bofya like hapa show love:

KHAMIS HK (Writer)

My Phone Number :+255718109106,

  • My TWITTER
  • My FACEBOOK

  • 0 comments:

    Proudly Powered by Blogger.
    back to top