Na Haruni Sanchawa
AFISA
Utamaduni Wilaya ya Ilala jijini Dar, Shani Kitogo amewaonya wenye baa
na pub kuzingatia sheria za nchi hasa wakati wa kufunga biashara zao.
Akizungumza
katika kikao cha pamoja kilichokaa hivi karibuni kwenye Ukumbi wa
Nyantare Tabata, afisa huyo alisema sheria lazima zizingatiwe.
“Uhalifu unasababishwa na watu wenyewe kwa kuwa hawazingatii sheria za nchi hasa wakati wa kufunga baa na pub.
“Ni
kosa kubwa kwa mmiliki yeyote wa baa au pub kutozingatia muda uliowekwa
wa kumaliza kazi zao kulingana na leseni yake ya biashara inavyosema,
hivyo nasisitiza kuwa ni lazima sheria hiyo ifuatwe,” alisema Kitogo.
Naye
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Baa Wilaya ya Ilala, Francis Msonga
alisema mikakati ya jeshi la polisi, Wilaya ya Kipolisi Buguruni ni
mfano wa kuigwa kwa wilaya na mikoa mingine.
Msonga aliyasema hayo
wakati wa kikao hicho maalumu kwa ajili ya kuweka hali ya usalama katika
maeneo yao ya biashara hasa mabaa yanayoonekana kuwa ni kero hasa
nyakati za usiku.
Aidha, mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ni jambo la
kujivunia kwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Buguruni, SP Jiliyo Simba
(pichani) kuitisha kikao hicho kwa lengo la kuwekana sawa.
Baadhi ya
wadau hasa wamiliki wa baa hizo wamesema kuwa jeshi la polisi
linajitahidi kufanya kazi zake lakini vitendea kazi havitoshi wakatoa
mfano kuwa wilaya nzima ya Buguruni ina magari mawili tu wakati matukio
yanaweza kuwa mengi kwa wakati mmoja.
Kamanda Simba alisema lengo la kikao hicho ni kuhakikisha watu na mali zao zinakuwa salama.
Wednesday, January 30, 2013
WENYE BAA DAR WAONYWA
Posted by WaChAfU INC
Tagged as: GAZETI LA UWAZI
4:43 AM
Share this Post
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BONYEZA ''LIKE'' HAPA
What they says
BONYEZA FOLLOW HAPA
Followers
MY FAVORITE BLOGS
Popular Posts
-
Huyu jamaa kwa upande wangu ni mtu wa maajabu sana maana kwenye hii ngoma amechana mbaya, sijui lkn labda ni kwa upande wangu isikilize...
-
click read more to download this. download here...!! umeipenda hii SHARE
-
Baada ya kutesa sana na kibao chake cha MAJANGA mwanadada SNURA sasa ameamua kuachia kigongo chengine kipya , mimi nakiita kigongo ma...
PROMO ONLY SONGS
G5CLICK
WaChAfU iNc. Powered by Blogger.
Social Icons
Download
Proudly Powered by Blogger.
0 comments: