Na Issakwisa Mponi
MWANAMKE
mmoja, Asia Ally Abeid (35 ) (pichani), mkazi wa mtaa wa Msikitini,
Buguruni kwa Mnyamani Dar, amefika katika Ofisi za Global Publishers Ltd
na kulia kwa uchungu akiwaomba Watanzania wamsaidie fedha za kulipia
vipimo na matibabu kutokana na uvimbe uliopo kifuani kwake.
Akizungumza kwa tabu, Asia aliyeambatana na mjomba wake alikuwa na haya ya kusema:
“Mwaka
2006, hiki kidonda na uvimbe unaouona kifuani, ulianza kama kipele
kidogo shingoni, taratibu ukakua huku ukiwa na maumivu makali. Nikaenda
hospitali ya Amana Ilala wakanipima na kuniambia kuwa ni uvimbe tu,
wakanifanyia upasuaji ili kuuondoa lakini baada ya muda uvimbe ukaanza
tena kurudi upya na kwa kasi zaidi ya mwanzo.
“Nilirudi tena
hospitali ya Amana mwaka 2009 ambapo walinifanyia upasuaji wa pili,
lakini jambo la kusikitisha baada ya muda mfupi tu, uvimbe ulianza
kurudi tena nikafanyiwa upasuaji mwaka 2010 katika hospitali ya Misheni
ya Maria Thomas iliyopo mjini Arusha, lakini pia haikusaidia kwani baada
ya muda uvimbe ulianza kurudi tena.
“Mwaka jana 2012, uvimbe ulikuwa
mkubwa kama unavyouona (ana muonyesha mwandishi kidonda), nikarudi
Hospitali ya Amana ambapo waliniambia wao wameshindwa hivyo
wakaniandikia niende Muhimbili ambako nilipimwa lakini hawakuona tatizo.
“Nimeambiwa niende Hospitali ya Aga Khan kwa kipimo kingine na gharama ni kubwa ni shilingi 450,000.
“Kwa
kuwa sina fedha hizo na ndugu zangu kutokuwa na uwezo wa kuzipata
nawaomba Watanzania wenzangu wanisaidi ili niweze kuokoa maisha yangu
yaliyo hatarini,” alisema mgonjwa huyo.
Wednesday, January 30, 2013
UVIMBE HUU UNANIUMIZA, NISAIDIENI JAMANI
Posted by WaChAfU INC
Tagged as: GAZETI LA UWAZI
4:42 AM
Share this Post
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BONYEZA ''LIKE'' HAPA
What they says
BONYEZA FOLLOW HAPA
Followers
MY FAVORITE BLOGS
Popular Posts
-
Huyu jamaa kwa upande wangu ni mtu wa maajabu sana maana kwenye hii ngoma amechana mbaya, sijui lkn labda ni kwa upande wangu isikilize...
-
click read more to download this. download here...!! umeipenda hii SHARE
-
Baada ya kutesa sana na kibao chake cha MAJANGA mwanadada SNURA sasa ameamua kuachia kigongo chengine kipya , mimi nakiita kigongo ma...
PROMO ONLY SONGS
G5CLICK
WaChAfU iNc. Powered by Blogger.
Social Icons
Download
Proudly Powered by Blogger.
0 comments: