Na Sofia Marcel
BABU wa Loliondo, Ambilikile Masapile ameambiwa aache kupambana na viongozi wa kiroho ambao ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Utetezi huo umetolewa na daktari wa binadamu wa Ukonga jijini Dar es
Salaam, Dk. Abdallah Mandai alipozungumza na gazeti hili mwishoni mwa
wiki iliyopita ambapo alisema Babu anapaswa kutambua kuwa watumishi hao
kazi yao ni kuwaelimisha binadamu wamtukuze na kumtambua Mungu tofauti
na yeye anayetumia tiba ya mitishamba.“Ipo tofauti kubwa, babu yeye kazi yake ni kutibu kwa njia ya asili, si kweli kwamba ana kikombe alichooteshwa, Mungu hawezi kutoa kikombe cha plastiki eti mtu atiie watu tena kwa fedha,” alisema Dk. Mandia.
Aliongeza kwamba Babu anapaswa kutambua kuwa uongo wake sasa umefikia mwisho: “Amedanganya na amepoteza wengi ambao wengine wamefariki dunia, sasa inatakiwa arudi kwa Mungu, atubu aliyoyafanya na siyo kuwadanyanga tena watu kwamba ana dawa nyingine.”
Aidha, Dk Mandia amesema Babu anatakiwa awaombe radhi Watanzania kwa kuwa ndugu zao wengi wamekunywa kikombe chake na hawakupona.
0 comments: