
KITUKO cha aina yake kimejiri Jumamosi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar wakati Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ ilipokuwa ikitumbuiza, Amani linakumegea kilichotokea.

Katika onesho hilo, Extra Bongo ilikuwa ikiwashindanisha mashabiki wake kucheza staili yao ya Kizigo na washindi kujinyakulia zawadi za fedha.
Wakati bendi hiyo inayoongozwa na ‘Kamarade’ Ally Choki ikitoa burudani, ghafla mwanamke huyo (jina lake halikupatikana) alivamia jukwaa na kuanza kucheza kwa staili aliyokuwa akiijua mwenyewe.

“Mimi ni mke wa mtu ukifanya mchezo nitakutolea laana,” alisema mwanamke huyo huku akizishika nguo zake na kuanza kuzitoa mwilini mwake moja baada ya nyingine.
Wakati mwanamke huyo akiendelea na zoezi lake la kusaula nguo, alijitokeza dada mwingine ambaye aliambatana naye pamoja ukumbini hapo na kumwita kwa jina la wifi.

Baada ya kuombwa sana na wifi yake, mwanamke huyo alivaa nguo zake na kuendelea na burudani hadi mwisho.
Haikufahamika mara moja kama mwanamke huyo alifanya kitendo hicho kutokana na pombe au hasira za kupigwa picha.
0 comments: