
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amezua jambo baada ya mume wa mtu, mkazi wa Kata ya Kwadelo wilayani Kondoa, Dodoma ambaye jina lake halikupatikana, kushindwa kuficha hisia zake za kimahaba na kuonesha waziwazi kumzimikia staa huyo.

Baada ya kupata nafasi ya kumuona Uwoya uso kwa uso katika maisha yake, mwanaume huyo alifanya jitihada za hali ya juu kujipenyeza katikati ya wanakijiji wenzake na kwenda kuweka pozi na staa huyo kisha kupiga naye picha huku akimkagua kuanzia ukucha hadi unywele.

Kwa mujibu wa wanakijiji wenzake, jamaa huyo alikuwa akitamba kuwa alimtaka Uwoya awe mkewe wa pili lakini aliishia kucheka tu bila kumkubalia wala kumkatalia kwa kuwa alimchukulia kama shabiki wake wa kawaida tu.
Katika tukio hilo, mbali na kuzindua Kilimo Kwanza, wasanii hao na Diwani Kariati, pia waliwakabidhi wanakijiji hao Sh. laki tano zilizotolewa kama pole na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Benard Membe kufuatia kijiji hicho kukumbwa na maafa ya mafuriko hivi karibuni.
0 comments: