LICHA ya kumwagana, mwigizaji mwenye mbwembwe nyingi kila kukicha ambaye ni mwajiriwa wa Kampuni Tuesday Enternment, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, amefunguka kuwa akitaka kujadili mambo ya mtoto aliyezaa na Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ huwa wanakwenda hotelini.

“Linapokuja suala la mtoto, huwa tunatafuta sehemu ambayo ni tulivu ili kujadili mambo ya mtoto. Tunakaa na kuongea mambo mbalimbali kwa ajili ya mtoto wetu, Salma,” alifunguka Kabula.

“Tukiwa hotelini na Chuz ni kwa ajili ya mtoto wetu maana sisi tukisikilizana, mtoto wetu atakuwa kwenye mazingira bora,” alisema Kabula kwa kujiamini.
Alipotafutwa Chuz ili kuthibitisha habari hizo, kilongalonga chake cha kiganjani kiliita bila kupokelewa.
0 comments: