9:38 AM
|
""NAOMBA MSAADA KWA RAISI, IGP MWEMA NA WANANCHI WOTE NIPATE HAKI ZANGU NIKIWA KAMA MAMA NA MKE KUFAHAMU KUJUA MUME WANGU ALIPO. |
|
Baada ya kukaa kwa siku mbili bila kujua alipo mume wangu, nimejitokeza
mbele ya waandishi wa habari wapate kunisaidia kufikisha ujumbe wangu wa
kupata msaada ya kujua mume wangu alipo. |
Hapa ni karibu kabisa ya ukumbi wa habari maelezo ambapo niliwafuata
waandishi wa habari ili kupata muda wa kuongea nao, nikiwa nimewabeba
wanangu Lincon na Linston.
|
Nina watoto wawili mkubwa ni wa miaka 2 na mdogo wake ni wa miezi 4, leo
ni siku ya nne hawajamuona baba yao, baba yao ni msaada mkubwa mno kwa
familia yangu, Raisi Kikwete huko ulipo nakuomba usikie kilio changu,
IGP Said Mwema nahitaji msaada wako, Wanawake na Wote nahitaji msaada
wenu. |
|
Hapa nikiendelea kuelezea hali halisi ya jambo hili mpaka leo hii kuja
hapa, na kubwa ni kutopewa taarifa ya mume wangu alipo. Sina Amani
kabisa naomba kupata taarifa kamili huko aliko yuko salama? na hata
kufahamu anakula nini?Kubwa watanzania wenzangu ni kunisaidia katika maombi ili huko aliko awe salama.
Kwa Urefu zaid habari hii itaruka katika vyombo mbalimbali vya habari
zikiwepo TV kama Channel Ten, ITV, EATV, Star TV na Clouds, Radio kama
Clouds, Radio One, na magazeti kama Mwananchi, Nipashe , Mtanzania,
Tanzania Daima , The Citizen, Guardian, na vyombo vingine vya habari.
Nawashukuru waandishi wote ambao walikuwepo hapa, pia na watanzania wote naamini mko pamoja na mimi.
| | | |
Share this Post
0 comments: