""Msipokuwa
wa kweli kwa kumshauri Fredi, radio yenu itakuwa na siku chache sana
kuwepo hai kwa kuwa radio yeyote inatemegemea watu na watu ni walewale
"wanaokwenda harusini ndio haohao wanaokwenda msibani" msiba wa Mangwea
umemgusa kila mdau wa muziki hasa vijana nyinyi kama radio/ukumbi (wadau
wa burudani) mnawaitaji na kuwategemea sana vijana katika kazi zenu,
kila msanii, kampuni zinazodili na vijana walihairisha show zao Nchi
nzima ili kuenzi na kuonyesha heshima kwa Ngwea/Bongofleva kasoro nyinyi
PLANET FM tu, huo sio uungwana wala utu na zaidi ukizingatia Ngwea ni
mtoto wa Morogoro na Mazishi yake yanafanyika hapa Morogoro,
mlichokifanya nyinyi PLANET FM ya morogoro ni sawa na matukio mawili
katika nyumba moja, yani nyumba hiyo hiyo moja (Moro) ina msiba halafu
nyinyi mkaweka harusi pia uliona wapi kama si uchuro, dhambi na matusi?
Mimi ningewezaje kuja ukumbini wakati ndio nasimama kama mwenyeji wa
wasanii na wadau wote wa burudani hapa Moro?
Ningeelewekaje kama King wa Bongo Flavour na hata watu wa Moro
wangaenionaje kama ningefanya show yenu ya jumamosi? Wanaokushangilia
leo ndio hao hao watakaokupiga mawe (watakuzomea) kesho kama ukiwakosea,
msipojitazama watu wanaweza kususia radio mpaka ukumbi wenu kwa
kuangalia pesa bila kujal utu, mfano ningekufa mimi Selemani, Mhando,
Warda, Fredi, Zombi, Frado n.k mngefanyaje hiyo show yenu? Je sisi
tunathamani kuliko Ngwea katika tasnia ya muziki wa bongofleva? Sasa
mitandao, radio, Tv, magazeti yakianza kuwachafua PLANET FM kwa kitendo
hicho mtapona? Hayo makampuni yatawapa tena matangazo na ukumbi wenu
watu wataendelea kuutumia kwa show? Mmesahau kuwa Moro wameshawai
kususia kila kitu cha Abood kuanzia mabasi, tv, radio n.k, kwa kutojali
kwake utu na kuangalia pesa tu? Mimi sikufika ukumbini nimefiwa kwa
kujali utu, kulinda heshima yangu, yenu na Moro kwa ujumla sasa kama
hamkunielewa mtakuwa mmechelewa sana na NINAAMINI HILI JAMBO HALITAPITA
KIMYAKIMYA BILA MITAA KUJUA UKWELI. Team amani na upendo"
0 comments: