Na Khatimu Naheka
KOCHA Mkuu wa Cameroon, Jean Paul
Akono amechukia kuona timu yake ikikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa
Taifa Stars lakini akataja sababu tatu zilizoleta kipigo hicho.
Hatua
hiyo ya Akono inakuja kufuatia Cameroon kukubali kichapo hicho
kilichotokana na bao la mshambuliaji Mbwana Samatta katika dakika ya 89
kwenye mchezo huo wa kirafiki uliopigwa juzi katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Akono alisema timu yake kuja kwa mafungu katika mchezo huo, pamoja na tofauti kubwa ya hali ya hewa iliyopo kati ya Tanzania na Cameroon ni kati ya sababu za kipigo.
Aliongeza kuwa mbali na matatizo hayo, uzembe wa mabeki wake kutegeana katika kuicheza krosi iliyozaa bao, nao ulichangia.
“Hatuwezi kujilaumu zaidi, nawapongeza Tanzania kwa kupata ushindi, wametupa kazi ya kufanya,” alisema Akono na kuongeza: “Hii ilikuwa mechi ya kirafiki na tunatakiwa tuichukulie kama sehemu ya kijifunza kutokana na makosa tuliyoyafanya.”
KWA HABARI ZAIDI ZA MICHEZO ni GAZETI LA CHAMPION
umeipenda hii SHARE
then comment
0 comments: