Na Khatimu Naheka
KIUNGO
mshambuliaji wa Yanga, Mganda, Hamis Kiiza (pichani), juzi alionyesha
uwezo mkubwa mazoezini na kufanikiwa kufunga mabao matatu ‘hat trick’.
Katika
mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Bora uliopo Kijitonyama
jijini Dar es Salaam, yakiwa ndiyo ya kwanza baada ya kuichakaza Prisons
kwa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa wikiendi
iliyopita, Kiiza alionekana kuwa na kiwango cha hali ya juu
kilichowafurahisha mashabiki waliohudhuria.
Mazoezi hayo
yaliyoshuhudiwa na Championi Jumatano yalianza kwa Kocha Mkuu, Ernie
Brandts, kuwahenyesha nyota wake kwa kupasha misuli muda mrefu.
Baada
ya kupasha misuli, Brandts aliwapumzisha nyota waliocheza kwa muda
mrefu kwenye mchezo dhidi ya Prisons na kubaki na wale wa akiba ambao
aliwagawanya katika vikosi viwili.
Kundi la kwanza lilikuwa na nyota
kama Juma Abdul, Kabange Twite, Ladislaus Mbogo, George Banda, David
Luhende, Godfrey Taita, Kiiza na Yusuph Abdul.
Lingine lilikuwa na
nyota kama Said Bahanuzi, Stephano Mwasyika, Nizar Khalfan, Omega Seme,
Shadrack Nsajigwa, Rehani Kibingu na Said Mohamed.
Timu ya akina Kiiza ilipata ushindi wa mabao 3-1, huku bao la kufutia machozi la ile nyingine likifungwa na Nizar.
Wednesday, January 30, 2013
Kiiza afufukia mazoezini Yanga!!
Posted by WaChAfU INC
Tagged as: GAZETI LA CHAMPION
5:15 AM
Share this Post
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BONYEZA ''LIKE'' HAPA
What they says
BONYEZA FOLLOW HAPA
Followers
MY FAVORITE BLOGS
Popular Posts
-
Huyu jamaa kwa upande wangu ni mtu wa maajabu sana maana kwenye hii ngoma amechana mbaya, sijui lkn labda ni kwa upande wangu isikilize...
-
click read more to download this. download here...!! umeipenda hii SHARE
-
Baada ya kutesa sana na kibao chake cha MAJANGA mwanadada SNURA sasa ameamua kuachia kigongo chengine kipya , mimi nakiita kigongo ma...
PROMO ONLY SONGS
G5CLICK
WaChAfU iNc. Powered by Blogger.
Social Icons
Download
Proudly Powered by Blogger.
0 comments: