LEO ngoja niongee na Jeshi la Polisi Tanzania, chini ya mkuu wake, IGP Said Mwema, hasa kitengo ambacho kinatoa umiliki wa silaha (bastola) kwa raia ambao huwa wanaomba ili wapewe idhini ya kuuziwa na kumiliki chombo hicho muhimu katika ulinzi.
Nimeamua
kuzungumza nanyi suala hili kutokana na staili ambayo inatumiwa na
baadhi ya watu mnaowamilikisha bastola kuwa wepesi wa kutoa silaha na
kuwapatia rafiki zao aidha wakapige nayo picha au waende nayo kwa
washikaji zao.
Hoja inakuwa hivi… kupiga picha ukiwa umeshika ‘mguu wa kuku’ tena ukiwa umejaa risasi ni fasheni?
Ndugu zangu wa Jeshi la Polisi, kwa staili hii kuna siku mtasikia kitu cha ajabu kupitia hizo bastola ambazo wamiliki wake hawafuati masharti ya umiliki wake.
Huko nyuma, hadi mtu ajulikane kuwa anamiliki bastola, ilikuwa mbinde kweli na hata ukijaribu kumuuliza mhusika kuwa eti mtaani inasemekana kuwa anamiliki chombo hicho, ilikuwa ni vigumu kukubali kirahisi lakini siku hizi imekuwa ni tofauti.
Utakuta mtu anajipiga picha kupitia simu yake ya mkononi akiwa ameshikilia bastola na kisha picha hiyo anaiweka katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter au BBM huku akiisindikiza na maneno ya ‘shombo’ yaliyojaa vitisho kwa raia.
Ukiachana na suala la mhusika ambaye anamiliki chombo hicho, kuna hili ambalo linanikera sana, eti mtu anampa bastola rafiki yake au mpenzi wake aende nayo kwa marafiki zake, klabu au sehemu mbalimbali za starehe ili kuwatisha watu kuwa naye ana ‘cha moto’.
Hii ni hatari sana kwa pande zote mbili, yaani kwa mmiliki na aliyeazimwa. Hatari yake inakuja pale mhusika, awe ameitumia vibaya hiyo silaha au aliyeazimwa aende kuitumia vibaya, unafikiri uchunguzi ukikamilika wangapi wataingia matatizoni?
Mwaka jana nilifanya mahojiano na rapa mdogo katika muziki wa Bongo Fleva, Abubakar Chende ‘Janjaro’ baada ya kusambaa kwa picha yake akiwa ameshikilia bastola, mbaya zaidi akiwa na umri wa chini ya miaka kumi na nane. Nilipombana akaniambia kuwa bastola hiyo alipewa na promota wake mmoja wa mkoani Dodoma ambaye alimpa ili akatanulie nayo.
Hatujakaa sawa, zikavuja tena picha nyingine za dogo huyohuyo akiwa ameshikilia bastola mkono wa kulia na mkono wa kushoto akiwa ameshikilia kifaa cha kuhifadhia risasi za bastola hiyo tena zikiwa zimejaa, nilipomuuliza akaniambia ni ya mwanamuziki mwenzake, Tunda Man ambaye huwa anampa bila kusema huwa anampa afanyie nini.
Siku chache baadaye, zikasambaa picha nyingine za mwanamuziki Nay wa Mitego akiwa ameshikilia bastola lakini yeye alipoulizwa alidai hajui aliitoa wapi na alipobanwa zaidi, akadai ni mali ya rafiki yake aliyegoma kumtaja.
Katika uchunguzi nilioufanya, niligundua kuwa bastola hiyo ilikuwa mali ya Tunda Man na niliporudi kwa Nay wa Mitego na kumueleza majibu ya uchunguzi wangu akabaki anacheka.
Hivi karibuni mwigizaji wa kike wa filamu za Kibongo, Isabella Mpanda, naye picha zake akiwa na bastola zilisambaa mtandaoni, alipoulizwa ni mali ya nani alidai ni ya rafiki yake ambaye ni mtoto wa aliyekuwa kigogo mkubwa katika Jeshi la Polisi enzi hizo ambaye ni mshikaji wa mchumba’ke, Luteni Kalama.
Yupo mwigizaji mwingine mkubwa wa filamu za Kibongo (jina tunalo) ambaye naye husifika kwa kuonesha mguu wa kuku kinyume na masharti ya umiliki wake.
Nimejaribu kutoa mifano hiyo michache na kuangalia hatari inayoweza kutokea endapo bastola hizo zitatumika vibaya. Je, suala hilo limekuwa fasheni kwa mastaa wetu? IGP Mwema kazi ni kwako kwani hawa mastaa wanataka kukuchezea sharubu. For the love of game!

0 comments: