FILM TRAILER CLOUDS 112 (DR MAX)

NEW VIDEO FREDRIGO - NAJIULIZA

Tuesday, September 24, 2013

SOMA MAKALA: WASANII WA ZANZIBAR WANAUA WENYEWE SANAA YAO:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
9:36 AM


Katika historia ya sanaa musiki tangu unanza kuchipua chipua Tanzania, basi utataja kote lkn huwezi kuacha kuitaja Zanzibar kwenye Nyanja hiyo, hata katika Nyanja ya sanaa za maigizo pia Zanzibar haikua nyuma kwa kipindi hicho cha nyuma,Makala yetu ya leo itahusisha sana wasanii wa filamu na musiki:Pichani ni Fey Honest anaefanya vizuri kwenye upande wa filamu, anaefuta ni Dorica, Sultan King, Baby j na Smile hao kwa upande wa bongo fleva:


Kama unayo kumbukumbu nzur utakumbuka michezo ya mwanzoni kuigizwa katika tape ni pamoja LOVE STORY TANGANYIKA NA UNGUJA ambayo ili actiwa na watu kutoka Tanga na Zanzibar, hii ni kabla kabisa ya kutoka filamu inayoitwa ya mwanzo  na vijana wa leo ya JOHARI iliyo igizwa na mastar RAY na MAREHEMU kanumba jijini Dar es salaam,


Licha ya kuwa cmbele kwa mambo yote hayo, Kipindi cha hii miaka ya karibuni Zanzibar imeonekana kushuka chini sana kwa viwango vya tasmnia zoe mbili Music Na Sanaa ya maigizo,


Tujaribu kuulizana Hivi Tatizo nini?? Wasanii wabunifu hamna kama wale wa zamani, au Dar 
kimeongezeka nini zaidi kiasi cha kushusha hadhi ya sanaa Zanzibar,tusitafute mchawi wachawi ni sisi wenyewe.

Leo Zanzibar kuna wasanii wengi tuu ambao wanakimbilia DAR- ES – SALAAM kwa ajili ya biashara hiyo, ni sawa tunasema wanafata soko ndo lilipo(Tuwaache leo tutawazungumzia siku nyingine),


 JE hawa waliyokuepo hapa wanafanya nini, au ndo wale wa ngoja na mimi niimbe na mimi mtaani wajue kama nimeingia studio,

Kiukweli  sanaa ya Zanzibar inauliwa na wasinii wenyewe mtake ama mistake hivyo ndo ilivyo:

Tunao hapa baadhi ya wasanii wa tasnia zote mbili Filamu NA music tunasema wanafanya vizuri lakini wanajulikana mwisho CHUMBE ukivuka ukimtaja basi hakuna anaemjua, Labda ajulikane na wasanii wenzake maana ndio wanao onana sana kwenye mitandao:


Pia wasanii wa Zanzibar hawaoneshi kuitumia mitandao ya kijamii kujitangaza km wafanyavyo 
wenzao, mfano Utakuata msanii kwenye wall yake ya FACEBOOK masalani anaandika Shit shit(ujinga ujinga) tuu, Anasahau km ana fanz wame muadd ilikujua yeye anafanya nini, yuko wapi na program anazofanya ni zipi, anashindwa kabisa kutambua ilo, pia waandish mbali mbali hutembelea facebook zao kujua leo nani kaandika nini lkn hawajui kabisa hilo:


Tuirejeshe Thamani a Sanaa ZANZIBAR asiyeweza akae pemben c lazima nyote muwe wasanii wengne mutachukuliwa kwenye Video Muuze sura, mnacho kifanya hakieleweki kabisa:


Kunapo kua na kibaya kizuri hakikosi wapo ambao wanajitahidi na wanajua nini wanafanya na pia wameeka sanaa kama ndio maisha yao, hao wanaweza kuiinua Sanaa ya ZANZIBAR ikiwa na wao Hawatalewa sifa na kuishia chumbe, Zanzibar ina wasanii wazuri tuu na wanaojua nini maana ya sanaa kikubwa ni kwamba baadhi yao hawajielewi wanatakiwa kufanya nini:

JIPANGENI: lego ni kutengeneza na si kubomoa:
haya ni mawazo yangu ya kwako toa hapo chini:

TOA MAONI YAKO HAPA:

KHAMIS HK (Writer)

My Phone Number :+255718109106,

  • My TWITTER
  • My FACEBOOK

  • 0 comments:

    Proudly Powered by Blogger.
    back to top