FILM TRAILER CLOUDS 112 (DR MAX)

NEW VIDEO FREDRIGO - NAJIULIZA

Thursday, July 25, 2013

ALICHOSEMA RAY C KUHUSIANA NA RECHO WA THT HIKI HAPA:

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
5:25 AM

Mwanamuziki wa kitambo Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ana matarajio ya kurudi katika game baada ya kuwa fiti sasa kiafya. Kupitia mtandao wa instragram Ray C amekuwa akitupia picha zinazomuonyesha akiwa na afya nzuri tena kanona si haba!

Watu wengi wamekuwa wakimuhoji kupitia mtandao huo kuhusiana na mwanamuziki Recho kutumia style inayofanana na Ray C kama anafurahia au lah huku kukiwa na nmafikirio huenda hapendezwi na kitu hicho lakini ukweli ni kuwa Ray C anamfurahia na hivi karibuni wanarajia kudondosha kolabo kwa mujibu wa alichokiandika Instagram.


Katika interview kadhaa Recho ameshawahi kukiri kuwa alivutiwa na Ray C kuingia katika muziki na ni mmoja katika ya wanamuziki anaowazimia mpaka leo na ndio maana style zao za  uimbaji na uchezaji zinafanana.Ray C pia aliwahi kuandika ujumbe wa kuwashukuru mashabiki wake kwa kumsapoti alipopata matatizo ya kiafya mpaka leo.

 Najaribu kuvuta picha ya kolabo ya wawili hawa halafu siipati hiyo picha yenyewe;

From SWAHILITZ
BOFYAHAPA
Facebook Twitter
YOUR COMMENT HERE:

KHAMIS HK (Writer)

My Phone Number :+255718109106,

  • My TWITTER
  • My FACEBOOK

  • 0 comments:

    Proudly Powered by Blogger.
    back to top