Kwa muda wa miezi kadhaa kumekuwepo
na bifu kali kati ya waigizaji wawili wa filamu Tanzania yaani Zena
Muhamed 'Shilole' pamoja na mwenzake Flora Mvungi. Kutokana na bifu hiyo
kufukuta kwa muda mrefu, Flora Mvungi na Shilole wameamua kuongea na
Hot Mix ya EATV ili kusahameana na kuanza upya safari yao ya maisha wakiwa huru
kama walivyokuwa hapo kabla.
I
Flora Mvungi ambaye alikuwa mkosaji ameweka bayana kwamba, baada ya
kukaa na kufikiria pamoja na kupata ushauri kutoka kwa ndugu, marafiki
pamoja na mashabiki wake, ameamua kuchukua uamuzi na hatua ili amuombe
Shilole msamaha kwa mambo ambayo aliyasema juu yake. Flora ameongeza
kwamba ameamua kuomba msamaha kwa muda wa wiki mbili sasa siyo kwa
Shilole tu bali hata kwa watu wengine ambao amewakwaza kwa namna moja
ama nyingine.
"Unajua kwa sasa naelekea katika ndoa na nimeshakuwa mtu mzima
sasa. Hivyo basi nataka niwe huru katika utu uzima wangu. Najua nlikosea
na ndiyo maana nimeamua kuja kumuomba Shilole rafiki yangu msamaha ili
tuishi kwa amani kama tulivyokuwa hapo awali" Flora alifafanua.
Shilole kwa upande wake amesema kwamba, haoni haja ya kuwa na bifu
na rafiki yake na ndio maana baada ya kumuomba msamaha alipokea na
kumuambia kwamba mpaka waende mbele za watu ambako Flora alitolea maneno
ya kashfa. Hivyo basi wakaamua kutinga ndani ya kituo cha televission cha EATV ili kusameana na
kuanza maisha mapya ya amani bila kinyongo kama walivyoishi awali.
Vilevile Shilole amedai kwamba, hajawahi kutoa maneno yoyote ya
kashfa dhidi ya Flora tangia wafahamiane. Hiimimemfanya kumuambia Flora
kama anahitaji msamaha wake lazima waende mbele ya jamii ili kuweka
hadharani na jamii pamoja na mashabiki kwa ujumla wafahamu hali
inayoendelea baina yao.
"Namuomba Flora kwamba, endapo atasikia jambo lolote ambalo
linaweza kumchonganisha na watu, asijichukulie hatua bila kumuona
mwenzake. Binadamu wala hila mbaya sana, kuna watu wanatunga maneno ili
kuwakosanisha. Hivyo basi kabla hujachukua hatua, basi kamuulize
mwenzako ili kama yanaweza kutatuliwa yatatulike" Shilole alimalizia na
kumbusu rafiki yake.
0 comments: