STAA wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ yamemkuta baada ya ile
ishu yake ya kutengeneza filamu inayoitwa Sister Marry ambapo mapadri
wamemtaka asiipeleke sokoni milele.
Ishu hiyo ilitokea kwenye kikao kizito cha saa 5 kilichofanyika
Jumanne iliyopita katika Ofisi za Utamaduni jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa kikao hicho walikuwa Ray, Mkurugenzi Mtendaji wa
Utamaduni aliyetajwa kwa jina moja la Mwansoke, mapadri wanne na mtu
mmoja aliyedaiwa kuwa ni wa kutoka Ofisi za Usalama wa Taifa.
Kikao hicho kilikuja baada ya hivi karibuni viongozi wa Kanisa
Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam kumtaka msanii huyo ajieleze
kimaandishi ni kwa nini mtawa Sister Marry (Irene Uwoya pichani) alikuwa
akifanya matendo ambayo kiuhalisia, Wakatoliki wenyewe huwa
hawayafanyi.
Kabla Ray hajajieleza kwa maandishi ndipo alipoitwa huko na
kukubaliana ana kwa ana na jopo hilo huku mashinikizo kadhaa
yakielekezwa kwake.
Awali, wajumbe wote wakiwa wamekaa
kwenye viti, filamu hiyo yenye saa
3 iliwekwa mwanzo mwisho huku mapadri hao wakiguna kila wakati, hasa
wakati Sister Marry akiwa anafanya mambo yake mabaya.
Baada ya kumalizika kwa filamu hiyo, hoja zikaanza. Mwansoke akasema
vipande vyote vichafu vinyofolewe na kubaki vile ambavyo wajumbe
hawakuvigunia.
Baada ya bosi huyo kusema hayo, mapadri wakasema ‘noooo’. Filamu hiyo
isiende mitaani hata kidogo kwani imejaa udhalilishaji wa Wakatoliki.
Inasemekana Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Maximilian Kolbe lililopo
Mwenge Kijijini (jina halikupatikana mara moja) yeye alipigilia msumari
wa mwisho kwa maneno aliyoyatoa.
Alisema kwa kuwa filamu hiyo ilirekodiwa kwenye kanisa lake hilo,
anataka vipande vyote vya kanisa hilo vitolewe ndipo iingie mtaani,
jambo ambalo lilimtoa machozi Ray.
Ray sasa! Siku ya Alhamisi iliyopita, Ray alizungumza na Amani na
kukiri kuwepo kwa kikao hicho. Akasema itakuwa vigumu kuviondoa vipande
vya kanisa hilo kwa sababu asilimia 85 ya filamu nzima imerekodiwa
Maximilian Kolbe.
“Asilimia 85 ya filamu imerekodiwa Maximilian Kolbe, sasa wanaposema
niviondoe ni kuimaliza filamu yote. Filamu ni ya saa 3, ukivitoa vipande
vya kanisa si itabaki dakika 5 tu,” alisema Ray.
Alisema kikao kiliisha kwa maamuzi hayo, kwamba mtu wa utamaduni
alisema vipande vichafu vinyofolewe huku mapadri wakitaka muvi nzima
isiende sokoni na paroko wa Maximilian Kolbe akitaka kanisa lake
lisionekane kwenye filamu hiyo.
Mwandishi: “Je, wewe Ray umeamuaje?”
Ray: “Sijaamua chochote kwa kweli. Niponipo tu, nimetumia fedha nyingi sana.”
Wednesday, January 30, 2013
Browse: Home
» MOVIES NEWS |BONGO MOVIES
» “FILAMU YA RAY IITWAYO “SISTER MARRY” YAPIGWA MARUFUKU NA MAASKOFU
“FILAMU YA RAY IITWAYO “SISTER MARRY” YAPIGWA MARUFUKU NA MAASKOFU
Posted by WaChAfU INC
Tagged as: MOVIES NEWS |BONGO MOVIES
4:07 AM
Share this Post
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BONYEZA ''LIKE'' HAPA
What they says
BONYEZA FOLLOW HAPA
Followers
MY FAVORITE BLOGS
Popular Posts
-
Huyu jamaa kwa upande wangu ni mtu wa maajabu sana maana kwenye hii ngoma amechana mbaya, sijui lkn labda ni kwa upande wangu isikilize...
-
click read more to download this. download here...!! umeipenda hii SHARE
-
Baada ya kutesa sana na kibao chake cha MAJANGA mwanadada SNURA sasa ameamua kuachia kigongo chengine kipya , mimi nakiita kigongo ma...
PROMO ONLY SONGS
G5CLICK
WaChAfU iNc. Powered by Blogger.
Social Icons
Download
Proudly Powered by Blogger.
0 comments: