FILM TRAILER CLOUDS 112 (DR MAX)

NEW VIDEO FREDRIGO - NAJIULIZA

Saturday, October 19, 2013

WIKI YA MAVAZI ZANZIBAR SOMA UJUE ITAKUAJE NA WAPI?

Posted by WaChAfU INC  
Tagged as:
4:04 AM

 (HABARI LEO)
TASNIA ya ubunifu wa mavazi inazidi kukua siku hadi siku nchini huku kukiwa na wadau mbalimbali ambao wanakuja na mawazo tofauti.
Kwa sasa, yapo maonesho makubwa ambayo yanasifika ndani na nje ya nchi na ambayo yametangaza kazi za wabunifu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania. Ubunifu wa mavazi ni tasnia ambayo inaweza kutangaza kwa kiasi kikubwa sifa za nchi kwa kuwa ni moja kati ya kazi za kiutamaduni.
Yapo maonesho makubwa kama vile Swahili Fashion Week, Maridadi Fashion Show, Ally Remtulah Show, Fashion Motomoto na nyinginezo. Katika maonesho hayo ya mavazi, yapo ambayo yanatumika kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia jamii kwa njia ya mnada ambapo mavazi yanauzwa na fedha kupatikana. Kwa sasa kuna onesho kubwa la mavazi ambalo ni Wiki ya Mavazi ya Zanzibar.
Onesho hili ni la kwanza kufanyika mwaka huu ambalo litafanyika kuanzia Oktoba 25 hadi 27. Ni onesho ambalo linashirikisha wabunifu wa mavazi kutoka ndani na nje ya Tanzania huku kukiwa na wageni mbalimbali ambao wanatarajia kuhudhuria. Zanzibar Fashion Week imetokana na mawazo ya wadau watatu wa masuala ya mitindo kisiwani humo ambao ni Adnan Abass, Faroque Abdella na Javed Jafferji.
Mratibu wa onesho hilo, Javed Jafferji anasema kuwa lengo la onesho hilo ni kuwaweka pamoja wabunifu wa mavazi ambao wanafanya kazi zao ndani na nje ya Zanzibar. Katika onesho hilo, kutakuwa na wabunifu mbalimbali kama vile Adam Hassan, Fatima Khamisi, Hasiba Quettawala, Ally Rehmtullah, Asia Idarous na Hameed Abdul.
Wengine ni Kanga Kabisa, Kihanga Designer, Made in Africa, Mama Momella, Maskat De Haan, Natasha Shyrose, Mago East Africa, Vida Mahimbo, Waiz Shelukindo, Upendo, Salaeh Sultan, Rizwan Jan Mohamed na wengineo wengi. Jafferji anasema onesho hilo litafanyika katika eneo la Mtoni Palace Ruins ambapo wabunifu wataonesha mitindo mbalimbali kama vile mitindo ya kisasa, kiutamaduni, vijana na ile ya watu watu wazima.
“Hii ni fursa kwao kuonesha uwezo wao katika fani ya ubunifu wa mavazi kwanza kuonesha kuwa wanaweza kutangaza kisiwa hiki nje ya mipaka yetu na pia kutangaza kazi zao pia na kujipatia soko,” anasema Jafferji. Anaongeza kuwa Oktoba 25, itakuwa ni siku ya ufunguzi wakati Oktoba 26 ndio itakuwa siku yenyewe ya onesho na Oktoba 27 ni kutakuwa na hafla fupi ya kufunga onesho.

TOA MAONI YAKO HAPA:
KWA MTAZAMO WAKO WEWE UNASEMAJE KUHUSU HILI;

Bofya like hapa show love:

KHAMIS HK (Writer)

My Phone Number :+255718109106,

  • My TWITTER
  • My FACEBOOK

  • 0 comments:

    Proudly Powered by Blogger.
    back to top