Mwanamusik wa miondoko mbali ya nchini T.Z HAMMER Q, leo ametoa somo kali kwa wale watumiaji wa madawa ya kulevya hapa nchini,na ambao wanafikiri utumiaji wa madawa ni kitu rahisi km kuingia na kutoka maliwatoni, aliamua kutoa somo hilo baada ya yeye kukutana na mwanadada muadhirika wa madawa hayo na kupewa stori nzima pamoja na kupewa onyo asijaribu hata siku moja kutumia...
hammer q aliamua kulitoa darsa hilo kupitia ukurasa wake wa facebook, kwa minajili ya kuwaonya na kuwaasa watu mbalimbali pamoja na mashabiki wake kuhusiana madawa..
statuz ya facebook aliyoiandika ya kutoa somo hilo ambayo ilipata wachangiaji wengi sana ni hii...!!!!
'''Ndugu zangu nawausia sana km ninavoiusia nafsi yangu starehe ya (UNGA) ni mbaya sana , leo nimepata bahati ya kukaa na mdada mmoja mrembo sana yy ni MTEJA wa unga amenipa story nying sana na za ukweli sana kuhusu maisha yake na uteja,kiukweli sio mzuri , cose mpaka analia jinsi alivokuwa ananielezea,ameniusia saaaaana nisijejaribu hata siku moja kuutumia na mungu aniepushie kabisa,na mimi nawaombeni sana sana kaeni mbali na hiyo starehe, na mungu atulinde na awatowe wale walioingia kwny shimo la uteja amin'''
je wewe unamaoni gani.....!!!???
0 comments: