
PICHA
za tukio la ‘bethidei’ ya mwanamitindo maarufu wa Bongo ambaye pia ni
Miss Tanzania 2001, Millen Magese ‘Happiness’ iliyofanyika hivi karibuni
huko New York, Marekani, ilikuwa ni kufuru tupu.
.

Kupitia
mtandao wa Instagram, modo huyo ambaye makazi yake ni Afrika Kusini
‘Sauzi’, aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kumpa sapoti ya kutosha
kwenye tukio hilo ambalo lilipewa jina la Birthday to Remember With
Super Modal Millen and Friend.


“Nawashukuru sana jamani, bethidei yangu ilikuwa baab’kubwa hivyo asanteni wote,” aliandika Millen mtandaoni.
Katika
pati hiyo, watu walijiachia kwa misosi kiwango, vinywaji vya bei mbaya
na kuserebuka muziki huku wakishindwa kuamini kama ni mrembo huyo
aliyeamua kuangusha sherehe hiyo.



habari imetoka GAZETI LA IJUMAA..
0 comments: